Sunday, April 28, 2013

NAMNA YA KUONDOA KIRUSI ANAEITWA "00Peuple_congolais,Ceci_nous_concerne_tous"

Hili ni Jina la Aina ya Virus hatari sana ambaye hukaa kwa removal devices hasa USB flashes na baadhi ya devices zingine kama simu na external

Huyu Virus ni HATARI sana kama anapokuwa kwenye device yako ukamRUN, moja kwa moja huenda kwa drive C:>\ na ktuengeneza makazi yake kule, kwa kutengeneza folder TATU hatari kama inavyoonekana hapa...kwa kawaida drive C: inapaswa kuwa na folder 4/5 tu ambazo ni USERS, PROGRAM FILES, WINDOWS, PERFLOGS, INTEL.......Intel  huweza kuwepo endapo graphic drivers zote zikikaa sawa

NDANI YA WIN32:SYSTEM folder kama inavyoonekana hapo juu, kuna file hizi hatari, kama unavyoziona hapa



SASA INAKUAJE/ COMPUTER INAHARIBIKA VIPI NA HUYU CONGOLAIS ????[/b]

Ndio swali ambalo complex hapa tuko kwa ajili ya kulijibu, Congolais baada ya kujitengenezea folders zake ambazo ni harmful, kitu anafanya ni kuua System32 ya computer yako ambayo ndo Root Folder ya Operating System <O.S> yako....So wakati mwingine unapoamua kuRUN hizo application ndipo OS yako inapoCORRUPT.

SASA ANTIVIRUS KAZI YAKE NINI????

Swali muhimu sana,ambalo Complex Tusingependa utange tange bila kujua tunafanyaje, Hii congolais virus ni hatari sana kwa kuwa imeandikwa kwa script ambazo ni VBEscript ambayo hii Hufanya kazi kupitia command form, kwa hiyo antivirus huweza kudetect madhara ya Congolaisie na sio virus yenyewe, kwa kuwa usipo IRUN hiyo virus haina madhara yoyote kwa computer yako....Kwa maana hiyo ANTIVIRUS iko safi na kazi zake,.....Ila nasuggest uwezo wa AVAST nilikwisha upima nkajionea.

JINSI YA KUMTOA HUYO VIRUS SASA???

Kwanza inakupasa kujua huyu virus yuko kwa device yako ipi e.g USB flash, External or etc. Sasa vizuri pia kujua device letter yako ni ipi mfano G: ama H: .......Baada ya hapo RUN command prompt kutoka kwa computer yako, click start alafu CMD itajitokeza hii application

Kisha Nenda kwa device yako ambayo inahuyo congolais virus, H:>\ 


Alafu baada ya Hapo andika "rename" kisha Bonyeza 00 kisha TAB button  ambayo iko juu ya CAPS LOCK ili yule virus ajiandike kama alivyo. kwenye cmd pale...mara zote anaishia na .vbe

Sasa baada ya kujiandika kama alivyo usibonyeze ENTER......Bonyeza SPACE kisha Bonyeza TAB button ambayo virus atajiandika tena kama alivyo.....then wewe futa ile .VBE pale mwisho kabisa andika .txt  kama inavyoonekana hapa


Baada ya Hapo, Virus wako atabadilika na atakuja kwa mfumo wa text file kwa device yako, baada ya hapo MFUTE kama unanawa vile.....Alafu nenda ka EMPTY recycle bin.......

NOTE:
Kama virus huyo alishatengeneza files zake kwa drive C: jiandae kufanya BACKUP ya data zako, na kufanya windows installations kwa kuwa haitachukua mda mref sana Operating system yako itacorrupt......

Karibu complex system kwa maswali na  maelekezo zaidi, ama kwa kupeana mawili matatu juu ya chochote karibu kwa forums zetu, ........Advanced Computing Skills




0 comments:

Post a Comment

Popular Posts